Home Kimataifa Dorcas Rigathi azindua miche Milioni 12 kaunti ya Nyeri

Dorcas Rigathi azindua miche Milioni 12 kaunti ya Nyeri

0

Mke wa Naibu Rais mchungaji Dorcas Rigathi, Leo Jumamosi amezindua awamu ya kwanza ya miche milioni 12 chini ya halmashauri ya maendeleo ya mto Tana na Athi (TARDA).

Uzinduzi huo uliotekelezwa katika wadi ya Kiamukuyu, eneo bunge la Mathira Magharibi kaunti ya Nyeri, utatekelezwa katika mwaka huu wa kifedha.

Mpango huo wa TARDA wa uzinduzi wa miche 12 ,unaambatana na agizo la Rais la upanzi wa miti bilioni 15 kufikia mwaka 2032.

Mchungaji Dorcas alitoa wito kwa wakenya kupanda miti, akisema kuwa misitu huenda ikatumiwa katika ufadhili wa Kimataifa.

“Changamoto nyingi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika, yanasababishwa na mataifa yaliyostawi, lakini hatuwezi hatutaendelea kulalamika, lazima tuchukue hatua,” alisema Dorcas.

Mwenyekiti wa halmashauri ya TARDA, Patrick Gichohi, alisema uzinduzi huo, unaashiria mwanzo wa upanzi wa miti milioni 12 iliyolengwa na TARDA.

“Tutapanda miti milioni 12 katika mwaka huu wa kifedha, ambapo kati ya miti hiyo,  540,000 itakuwa miti ya matunda,” alisema Gichohi.

Wakati wa uzinduzi huo, miche 21,000 ilisambazwa kwa watu, mingine ikipandwa katika wadi ya Kirimukuyu.

Website | + posts