Home Habari Kuu Dorcas: Familia zinapaswa kuwa msingi wa kushughulikia afya ya akili

Dorcas: Familia zinapaswa kuwa msingi wa kushughulikia afya ya akili

0

Mchugaji Dorcas Rigathi ameelezea umuhimu wa jukumu la familia katika kushughulikia afya ya akili.

Akizungumza wakati wa kongamano kuhusu afya ya akili Jijini Nairobi, Dorcas alisikitika kuwa barani Afrika afya ya akili haijaeleweka vyema hasa katika familia.

“Barani Afrika, afya ya akili haijaeleweka vyema. Unapokuwa na mzazi mgomvi, ndugu mwenye vurugu au binamu na bintiamu walio na hasira, huwa hatuangalii chanzo cha tabia hizo zao. Wakati mwingine tunawatenga na hivyo kusababisha hali zao ya kiakili¬† kuwa mbaya zaid,” alisema Dorcas.

Mchungaji Dorcas alitoa wito kwa waajiri kushughulikia afya ya akili wa wafanyikazi wao, ili kuhakikisha taifa lenye nguvu kazi na pia katika sekta ya kibinafsi.

Kaimu afisa mkuu mtendaji wa halmashauri ya kukabiliana na utumizi wa mihadarati (NACADA),  Prof.John Muteti, alisifu hatua zilizochukuliwa na mchungaji Dorcas katika vita dhidi ya migadarati, hasaa katika eneo la pwani ambalo limeathirika zaidi na utumizi wa mihadarati.

Prof Muteti alisema ripoti iliyozinduliwa hivi majuzi na NACADA, ilidokeza ongezeko la utumizi wa bangi hapa nchini.

Muteti alisema utumizi wa bangi hapa nchini umeongezeka maradufu katika muda wa miaka mitano iliyopita.

Website | + posts