Home Kimataifa Dkt. Nyambura Ndung’u: Nitafanikisha utendakazi wa shirika la KBC

Dkt. Nyambura Ndung’u: Nitafanikisha utendakazi wa shirika la KBC

Dkt. Nyambura alihakikishia sekta ya vyombo vya habari nchini kuwa hataingilia katika shughuli zao.

0
Waziri mteule wa Habari na Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali Dkt Margaret Nyambura Ndung’u.
kra

Waziri mteule wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali Dkt Margaret Nyambura Ndung’u, anaamini kuwa shirika la utangazaji nchini KBC lina rasilimali za kutosha kufanikisha utendakazi wake.

Dkt. Nyambura ambaye alikuwa akisailiwa na kamati ya bunge kuhusu uteuzi siku ya Ijumaa, alisema shirika la KBC linaweza kuboresha utendakazi wake na kuchangia pakubwa ustawi wa taifa hili.

kra

“Kile kinachojiri sasa ni teknolojia ibuka, na shirika hilo halijakuwa na kasi ikilinganishwa na vyombo vya habari vya kibinafsi,” alisema Dkt. Nyambura.

Iwapo ataidhinishwa katika wadhifa huo, Dkt. Nyambura alisema anapania kuhakikisha kwamba shirika la utangazaji la KBC, linashirikiana na vyombo vingine vya habari katika matumizi ya miundomsingi yake kwa manufaa ya taifa hili.

Dkt. Nyambura pia alihakikishia sekta ya vyombo vya habari nchini kuwa hataingilia katika shughuli zao.

Hatahivyo alisema sekta ya habari lazima iwajibike inaposambaza habari kwa umma.

Website | + posts