Home Kimataifa Dkt. Karanja: Nitawaangamiza walaghai katika wizara ya Kilimo

Dkt. Karanja: Nitawaangamiza walaghai katika wizara ya Kilimo

Waziri huyo mteule wa kilimo, alisema atabuni mikakati ya kutathmini mchakato wa ununuzi na usambazaji wa mbolea kupitia asasi za serikali.

0
Waziri mteule wa kilimo Dkt. Andrew Karanja.
kra

Waziri mteule wa kilimo Dkt. Andrew Muhia Karanja, ameahidi kuangamiza ufisadi na makundi ya walaghai katika wizara hiyo, iwapo uteuzi wake utaidhinishwa.

Alipofika mbele ya kamati ya bunge la taifa kuhusu uteuzi Ijumaa asubuhi, Dkt. Karanja alisema iwapo atachukua hatamu za uongozi katika wizara hiyo, atahakikisha walaghai wote wametokomezwa, ili kuwawezesha wakulima kupata pembejeo za kilimo za ubora wa hali ya juu.

kra

“Nafahamu kukabiliana na makundi ya walaghai ni swala ngumu, lakini iwapo uteuzi wangu utaidhinishwa, natoa ilani kwa walaghai hao. Ninashikilia maadili ya hali ya juu zaidi. nitakabiliana nao,” alisema Dkt. Karanja.

Wakati huo huo waziri huyo mteule wa kilimo, alisema atabuni mikakati ya kutathmini mchakato wa ununuzi na usambazaji wa mbolea kupitia asasi za serikali, kama vile shirika la kukadiria ubora wa bidhaa, kuhakikisha viwango bora vinaafikiwa.

“Nitahakikisha uwazi na maadili yanatekelezwa katika mchakato wa ununuzi wa pembejeo za kilimo,” aliongeza Dkt. Karanja.

Aidhi Dkt. alitupilia mbali madai kwamba awali alihudumu kama msaidizi wa kibinafsi wa waziri wa zamani wa kilimo Mithika Linturi.

Kiongozi wa wengi katika bunge la taifa aliye pia mbunge wa Kikuyu Ichung’wah, alimtaka waziri huyo mteule kufafanua madai ya uhusiano kati yake na Linturi.