Dirisha refu la uhamisho wachezaji katika ligi kuu ya Kenya,FKF linatarajiwa kufungwa leo usiku wa manane, huku shirikisho la kandanda likitoa siku 10 kwa kila timu kuwasilisha stakabadhi za uhamisho huo.
Ligi kuu ya FKF msimu wa mwaka 2024/2025 itarajea mwishoni mwa juma hili, baada ya mapumziko ya kutoa fursa kwa mechi za kimataifa.
usajili wa wachezaji umekuwa ukiendelea kwa miezi miwili iliyopita huku vilabu vikinoa makali yao tayari kwa msimu mpya ulioanza wiki mbili zilizopita.
Takriban wachezaji 120 wamesajiliwa kutoka humu nchini au nje ya nchi, huku zaidi ya 100, wakihamia mataifa mengine au vilabu vinavyoshiriki ligi ya daraja ya kwanza NLS.
Tusker FC ndio timu iliyowasajili wanandinga wengi zaidi wakiwa 10 huku ikiwatema 13 nao Gora Mahia FC na Murang’a Seal,Mathare United na Kenya Commercial Bank zimewasajili wachezaji watano kila moja wakati AFC Leopards ikiwanasa wachezaji wanne.