Home Kimataifa Diplomasia ya China kwa mwaka 2024 itaendelea kuwa ya kuhimiza amani duniani...

Diplomasia ya China kwa mwaka 2024 itaendelea kuwa ya kuhimiza amani duniani na kuleta mambo ya kisasa

0

Kwa kipindi kirefu sasa sera ya mambo ya China imekuwa ni sera inayozingatia kanuni ya kujiamini na kujitegemea, uwazi na ushirikishwaji, haki na ushirikiano, na kutafuta njia za pamoja za kutatua changamoto mbalimbali duniani.

Sera hii imekuwa endelevu, na msingi wake umekuwa imara, lakini huwa na marekebisho madogo madogo kulingana na mazingira ya diplomasia dunia na mahitaji ya siasa za kimataifa.

Kwa mwaka huu mpya wa 2024, moja ya mambo muhimu yanayojulikana ni kwamba China itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na hali ya sintofahamu inayoongezeka na kutekeleza jukumu lake kama injini ya kuleta amani na utulivu duniani.

Dunia iliingia mwaka 2024 kukiwa na changamoto mbalimbali duniani, kama vile mgogoro kati ya Russia na Ukraine na ule kati Israel na kundi la Hamas.

Migogoro hii miwili sio kama tu imeleta utatanishi iwe ni kwenye masuala ya amani, wakimbizi na hata kwenye diplomasia ya kimataifa kwa ujumla, bali pia imeonesha sura hali ya nchi ipi inafanya nini kwenye migogoro duniani.

Sio siri kuwa Marekani ni kigogo kwenye maswala ya diplomasia duniani, lakini tukiangalia mambo inayofanya Marekani kwenye migogoro hiyo miwili, tunaweza kuona kuwa inachochea migogoro hiyo na kutumia nchi zinazoshiriki kujinufaisha kisiasa na kiuchumi, lakini watu wa kawaida kwenye nchi hizo wanakumbwa na taabu nyingi na machungu.

Marekani imekuwa ikiihimza Ukraine iendelee kupambana na Russia na hata kuipatia fedha na silaha huku ikizishawishi nchi nyingine za magharibi zifanye hivyo.

Marekani imekuwa ikifanya hivyo hata kwenye mgogoro kati ya Israel na kundi la Hamas, na kufumbia macho kwa makusudi mauaji yanayofanyika Gaza Lakini China kwa upande mwingine imekuwa na msimamo wazi kuwa utatuzi wa migogoro hiyo unatakiwa kufanya kwa njia ya mazungumzo, na unatakiwa kuzingatia haki na maswala yanayofuatiliwa na kila upande, na pia kuhakikisha kuwa migogoro hiyo haiathiri uchumi na maisha ya watu.

Sauti ya China kwenye mambo ya kidiplomasia duniani inaonekana kuwa ni sauti ya busara, na bila uingiliaji na uchochezi wa baadhi ya nchi za magharibi sera ya mambo ya nje ya China imeonekana kuwa na ufanisi.

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alitoa mifano kadhaa kuhusu baadhi ya mambo iliyofanya China kwa mwaka jana ikiwa ni pamoja na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, (kwa maana ya maendeleo ya mmoja yawe na manufaa kwa mwingine), kufanyika kwa mkutano mkuu wa tatu “Ukanda Mmoja, Njia moja”, upanuzi wa kundi la BRICS, Mkutano wa kilele wa China na Asia ya Kati, na kufanikishwa kurudishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Saudi Arabia na Iran.

Tukiangalia shughuli hizo zote za kidiplomasia tunaona kuwa inachofanya China ni kushirikisha wadau mbalimbali kwenye maendeleo, na kutaka pande shiriki pia zinufaike na maendeleo ya China, hii ni tofauti na pande zinazopenda kuona kuwa migogoro inanufaisha malengo yake ya kimkakati na kiuchumi.