Home Burudani Dhiki ya Simple Boy yaleta faraja

Dhiki ya Simple Boy yaleta faraja

0

Msanii Stephen Otieno Adera maarufu kama Stevo Simple Boy sasa ana kila sababu ya kutabasamu baada ya mbunge wa eneo la Mumias Mashariki Peter Salasya kutimiza ahadi yake.

Mbunge huyo amemkombolea msanii huyo na mke wake nyumba alivyoahidi.

Akizungumza na mwanahabari mmoja wa mitandaoni, Salasya alielezea kwamba amelipa kodi ya nyumba hiyo na anapanga kumpeleka mke wa Simple Boy akasomee kozi fupi ya urembo. Baada ya kukamilisha kozi hiyo mbunge Salasya atamfungulia biashara.

Alipoulizwa sababu ya kuamua kumsaidia Simple Boy, Salasya alisema anakumbuka wakati alikuwa katika hali kama ya msanii huyo na hakupata usaidizi.

Simple Boy alikutana pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hakimiliki za Muziki Nchini, MCSK Dkt. Ezekiel Mutua.

Mutua alichapisha picha akiwa na msanii huyo na kuelezea kwamba walishiriki chamcha na kujadiliana kuhusu usaidizi anaohitaji ili kujiendeleza kama msanii.

Mke wa Simple Boy alifichua kwamba walikuwa fukara ilhali mume wake alikuwa na usimamizi ambao alidai haukuwa unawajibika.

Kampuni iliyokuwa ikimsimamia Simple Boy ya Men in Business baadaye ilitangaza kukatika kwa mkataba kati yake na msanii huyo.

Sasa amesema yuko tayari kujisimamia mwenyewe akisaidiwa na marafiki.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here