Home Burudani Desagu: Sina uhusiano na Matara!

Desagu: Sina uhusiano na Matara!

0

Mchekeshaji na mwigizaji wa mitandaoni Henry Desagu amesema kwamba yeye hana uhusiano wowote wa kiukoo na mshukiwa wa mauaji John Matara.

Desagu alichapisha picha ya Matara kwenye akaunti yake ya Instagram na kuandika, “Sina uhusiano na jamaa anaitwa John Matara. Yeyote anayeniambatanisha naye anafaa kupuuzwa.”

Hii ni baada ya watumizi wa mitandao nchini Kenya kuanzisha uvumi huo kutokana na namna ambayo wawili hao wanafanana.

Matara amezungumziwa sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na mauaji ya Starlet Wahu Mwangi ambapo yeye ndiye mshukiwa mkuu.

Tangu kisa hicho kilipotokea na Matara kutiwa mbaroni, wanadada wengi wamejitokeza kudai kwamba waliwahi kudhulumiwa naye.

Mmoja wao alielezea kwamba walikutana kwenye jukwaa moja la kukutanisha wapenzi mitandaoni na akawa anamtumia pesa nyingi.

Siku ya kukutana wakakodisha nyumba ambapo wakutana ili kuburudishana, anasema kila kitu kilikuwa sawa hasi usiku wa manane wakati Matara alibadilika ghafla.

Anasema alianza kumpiga huku akitaka amtumie pesa zote alizokuwa nazo kwenye akaunti zake na baadaye akamlazimisha awasiliane na ndugu jamaa na marafiki wamtumie pesa.

Alipotosheka na kiwango ambacho alikuwa amepata alimwacha kwenye nyumba hiyo akiwa amemfunga na aliokolewa na mama ambaye alikuwa amekuja kusafisha nyumba hiyo.

Maafisa wa upelelezi wa jinai wanaendeleza uchunguzi ili kubaini iwapo amekuwa akitekeleza mauaji kwa njia sawia.

Website | + posts