Mwanamitandao Milicent Aywa almaarufu Dem wa facebook alionekana kupandwa na mori kutokana na vitendo vya wasanii wa nyumbani kwao Kitale.
Wasanii hao ambao awali walianzisha kampeni mitandaoni ya kukana hafla alizokuwa amepanga Milicent walimfumania Obinna ambaye hufanya kazi na Dem wa Facebook wakitaka kujumuishwa kwenye onyesho hilo.
Video iliyosambazwa mitandaoni ilionyesha wasanii hao wakiwa wamezingira gari ya Obinna wakitaka kuzungumza naye huku wakilalamika kwamba aliwarejelea kama wasanii wa mtaani.
Kulingana na Obinna mmoja wa wasanii hao alimtukana akitafuta kile alichokitaja kuwa “haki yake” ya kujumuishwa kwenye tamasha na baadaye alipwe.
Msanii huyo alionekana kughadhabishwa na usemi wa Obinna akisema yeye sio msanii wa mtaani, alipoulizwa iwapo yeye ni wa kimataifa akaonekana kuchanganyikiwa.
Katika kikao na wasanii hao, Millicent aliwakosoa akisema wamekasirisha mkubwa wake kikazi ambaye amempa fursa ya kukua katika fani yake na ndio mara ya kwanza amempeleka nyumbani.
“Hayo matusi mmetusi Obinna mngeniwekea mimi. Mimi ndio msichana wenu wa nyumbani, sio Obinna. Obinna ni mkubwa wangu.” alisema Dem wa Facebook.
Inaaminika kwamba waliafikiana kwani usiku wa jana video ilisambazwa ikionyesha wasanii hao jukwaani ila umati uliokuwepo haukuridhishwa na tumbuizo lao.