Home Kimataifa DCI yapokea tarakilishi kutoka kwa serikali ya Ujerumani

DCI yapokea tarakilishi kutoka kwa serikali ya Ujerumani

Akipokea vifaa hivyo, mkurugenzi wa DCI Mohamed Amin alishukuru ubalozi wa Ujerumani kwa msaada wake mkubwa kwa kitengo hicho

0
kra

Serikali ya Ujerumaini imeimarisha maabara ya tarakilishi ya kitengo cha upelelezi cha DCI kwa msaada wa tarakilishi 30.

Kwenye taarifa, DCI ilisema vifaa hivyo vilitolewa na balozi wa Ujerumani nchini Sebastian Groth, kwenye hafla iliyoandaliwa katika chuo cha kitaifa cha mafunzo ya upelelezi jana Alhamisi.

kra

Akipokea vifaa hivyo, mkurugenzi wa DCI Mohamed Amin aliushukuru ubalozi wa Ujerumani kwa msaada wake mkubwa kwa kitengo hicho ambao umechangia pakubwa katika kuimarisha utendakazi wa maafisa wa DCI.

Ujerumani yakabidhi DCI maabara ya tarakilishi.

Aliongeza kuwa kupitia msaada wa serikali ya Ujerumani, maafisa hao sasa wameimarisha ujuzi wao wa kuchunguza kila aina ya uhalifu.

Kwa upande wake, Groth alipongeza ushirikiano ulioko baina ya mashirika ya upelelezi ya Kenya na Ujerumani akiutaja kuwa  muhimu katika kudumisha amani na usalama wa umma.