Home Habari Kuu DCI yapachisha picha za majambazi sugu wanaotafutwa na polisi

DCI yapachisha picha za majambazi sugu wanaotafutwa na polisi

Kulingana na idara ya DCI kupitia mtandao wa X siku ya Ijumaa, huenda majambazi hao wamejihami na ni hatari kwa wananchi.

0

Maafisa wa polisi wa upelelezi wa jinai DCI, wamechapisha picha za majambazi sugu ambao wako mbioni baada ya kumshambulia afisa mmoja wa polisi Kaunti ya Siaya.

Afisa huyo wa polisi alikuwa miongoni mwa maafisa waliokuwa wakisimamia mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE.

Kulingana na idara ya DCI kupitia mtandao wa X siku ya Ijumaa, huenda majambazi hao wamejihami na ni hatari kwa wananchi.

” Washukiwa hao waliotoroka mtego wa polisi tarehe 22 mwezi Novemba mwaka 2023, katika Kijiji cha Nina,” ilisema idara ya DCI

Mnamo tarehe 20 mwezi Novemba, afisa huyo wa polisi aliuawa kwa kudungwa kisu,huku bunduki yake na Ile ya mwenzake zikiibwa, walipokuwa wakipeleka makaratasi ya mtihani wa KCSE katika eneo la Mahero.

Polisi waliaandama washukiwa hao na kuwaua wawili na kupata bunduki mbili.

Idara ya DCI imetoa wito kwa wananchi kutoa habari kwa polisi kuhusu washukiwa hao kupitia nambari isiyo na malipo  0800722203.

Website | + posts