Home Taifa DCI yaapa kuwakamata waporaji wakati wa maandamano

DCI yaapa kuwakamata waporaji wakati wa maandamano

0
kra

Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI imeapa kuwakamata watu wote waliohusika katika visa vya uporaji wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024 wiki jana. 

Idara hiyo imechapisha picha za washukiwa zilizonaswa kwenye kamera za CCTV na kutoa wito kwa umma kuisaidia kuwatambua washukiwa hao ili hatua ichukuliwe dhidi yao.

kra

“Ingawa baadhi yao tayari wamekamatwa na kufikishwa mahakamani leo, wengine wengi bado hawajakamatwa na wanasubiri wakati mwafaka ili kupora tena na kusababisha madhara zaidi na kuhatarisha maisha ya Wakenya wasiokuwa na hatia,” imesema DCI katika taarifa.

“Tunaweza tukawakamata kutoka miongoni mwetu kwa sababu hawashirikishani kanuni sawa na zile zinazoelezea kile tunachosimamia, na hasa kwa wale ambao hawakustahili kupoteza kitega uchumi chao cha pekee katika hali hii.”

DCI imewataka Wakenya kupiga ripoti kwa kituo cha polisi kilicho karibu nao kuhusiana na walipo washukiwa au kupiga simu kupitia nambari ya simu isiyotozwa malipo ambayo ni 0800 722 203.

Wakati wa mahojiano jana Jumapili, Rais William Ruto alisema wahalifu walitumia maandamano ya vijana wa Gen Z kupora mali na kusababisha hasara ya mamilioni ya pesa na kuapa kuhakikisha kwamba wanakabiliwa na mkono mrefu wa sheria.