Home Biashara David Kibet Kemei ateuliwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya ushindani nchini

David Kibet Kemei ateuliwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya ushindani nchini

0
kra

Aliyekuwa mwenyekiti wa kampuni ya kutoa bima kwa kampuni za bima Kenya Re David Kibet Kemei ameteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya ushindani nchini na sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge.

Atakapoidhinishwa na kamati ya bunge kuhusu fedha na mipango ya kitaifa pamoja na ile ya bunge la seneti,Kemei atachukua mahala pa Adano W. Rioba, ambaye amekuwa akihudumu kama kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo tangu mwaka 2023.

kra

Spika wa bunge Moses wetangula alijuza wabunge jana kwamba kaimu waziri alikuwa amemteua Kemei kwa wadhifa huo na alikuwa anatafuta kuidhinishwa kwake na bunge.

David Kibet Kemei ana shahada ya biashara katika masuala ya uhasibu na shahada ya uzamili katika usimamizi wa biashara kutoka chuo kikuu cha Nairobi.

Taaluma yake ilianza mwaka 1990 alipohudumu kama mwanagenzi kwenye shirika la kitaifa la biashara – Kenya National Trading Corporation.

Baadaye alifunza katika chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kufanya kazi katika mashirika kama Nation Media Group, Windsor Golf Hotels and Country Club na tume inayosimamia kawi nchini Energy Regulatory Commission.

Website | + posts