Home Burudani Dave Chappelle wa Marekani akataa simu kwenye onyesho lake nchini

Dave Chappelle wa Marekani akataa simu kwenye onyesho lake nchini

0

Mcheshi maarufu kutoka Marekani Dave Chappelle, amewaduwaza wapenzi wa Sanaa hiyo wa humu nchini walio na kiu ya ucheshi wake kuwa hawataruhusiwa kuingia na simu kwenye onyesho la leo ukumbini Louis Leakey jijini Nairobi.

Ujio wa Chappelle umeonekana kupokelewa kwa hamu kubwa kwani tiketi za shilingi 7,000 kila moja ziliuzwa zote Kwa muda wa masaa mawili tangu kutangazwa kwake na waandalizi: Punchline Comedy Club.

Hata hivyo, swala la simu limebaki swali kuu kutokana na mazoea ya wakenya kuitumia kwenye maonyesho mengi ya humu nchini na hata ughaibumi.

Kwa mujibu wa Dave, ukosefu wa simu hufanya hadhira kuwa makini na kushiriki katika maigizo yake.Mazingira haya humpa msukumo wa kuchekesha zaidi.

Vile vile, watu wengi hupenda kupiga picha, kunakili sauti na kurekodi video kisha kusambaza kwenye mitandao kinyume na mapenzi ya waigizaji wengi hivyo kupelekea ubunifu kuibwa au kuigwa. Jambo hili linamuchukiza Chappelle.

Zaidi ya hayo, Kuna wale wenye kasumba ya kueneza habari za Siri za hadhira kwa kuwapiga picha na kuzitumia vibaya hivyo kufanya watu wengine kukosa amani wakati wa maigizo.

Kwa mujibu wa wafuasi wake wa karibu, swala la kupiga simu marufuku sio geni kama inavyodhaniwa na wengi bali ni mutindo wake. Kule Florida nchini Marekani, aliondoka jukwaani alipoona mtazamaji mmoja akitumia simu.

Mambo muhimu kuhusu Chappelle.

Alianza ucheshi wa stand-up akiwa na umri wa miaka 14.

Ana miliki onyesho maarufu la Chappelle.

Alikataa mkataba wa donge la pauni milioni 50 na Central Comedy mwaka wa 2005.

Alikubali mkataba wa Stand-up special 2016 na Netflix kwa pauni milioni 60.

Ameshinda mataji mengi ya Emmy na Grammy kutokana na ucheshi.

Huangazia siasa, rangi na maisha ya kijamii kwenye ucheshi wake.

Huwapa maskini misaada na pia ni mwana harakati.

Boniface Mutotsi
+ posts