Home Burudani Crazy Kennar azidiwa na hisia alipotangaza kifo cha mwanawe

Crazy Kennar azidiwa na hisia alipotangaza kifo cha mwanawe

0

Mchekeshaji na mwigizaji Crazy Kennar ametangaza kifo cha mwanawe wa kiume. Hakutoa maelezo zaidi lakini alisema aliaga dunia siku 4 kabla ya onyesho lake.

Akizungumza wakati wa kufunga onyesho hilo kwa jina “Happy Country” jana jioni katika jumba la KICC, Kennar alisema alikuwa na wakati mgumu kupanga onyesho hilo akiwa amefiwa na mwanawe.

“Kwa bahati mbaya, mwanangu aliaga dunia siku 4 zilizopita, imekuwa safari ngumu kwangu kwa sababu ilibidi tupitie hilo huku tukipanga onyesho.” alielezea Kennar huku akiwa amejawa hisia.

Alihimiza waliokuwepo kujizoesha kujulia wenzao hali hata kama wanatembea wakitabasamu huenda wanapitia matatizo.

Mchekeshaji huyo aijawa na hisia pia wakati wa kuaga baada ya onyesho kutokana na namna ambayo onyesho hilo lilifanikiwa pakubwa.

Alikumbatia wahusika wote wa onyesho hilo jukwaani wakiwemo Sandra Dacha, Jackie Vike na Osoro na mwisho anaonekana akitokwa machozi.

Alikaribisha waliokuwepo kwa “Happy Country” ishara kwamba huenda akaandaa tamasha sawia kila mara.

Website | + posts