Home Habari Kuu COWU yakiri mwaka 2023 ulikuwa mgumu kwa wafanyakazi

COWU yakiri mwaka 2023 ulikuwa mgumu kwa wafanyakazi

0

Chama cha wafanyakazi katika sekta ya mawasiliano nchini, COWU kimekiri kuwa mwaka 2023, umekuwa mgumu kwa wafanyakazi wote nchini Kenya kutokana na matozo mapya ya serikali na kupanda kwa gharama ya maisha.

Kwenye mahojiano na shirika la KBC, Okwaro ameitaka serikali kutafuta mbinu za kuwaondolea wafanyakazi mzigo mwaka ujao ikiwemo kuwapa nyongeza ya mishahara.

Okwaro ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa COTU ametaja mwaka 2023 kuwa mgumu baada ya tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi, SRC kukataa kutekeleza baadhi ya nyongeza iliyopendekezwa na vyama vya wafanyakazi nchini.