Home Kimataifa COTU yamshauri Mbadi kutokubali masharti ya IMF moja kwa moja

COTU yamshauri Mbadi kutokubali masharti ya IMF moja kwa moja

0
kra

Muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini COTU umemshauri waziri mpya wa fedha John Mbadi kutokubali na kutotekeleza masharti ya shirika la fedha la kimataifa IMF bila kuyazingatia.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli, muungano huo unasema ushauri wao unatokana na utawala wa Rais Mwai Kibaki.

kra

Utawala huo kulingana na COTU ulizingatia sana maslahi ya wananchi kabla ya kutekeleza moja kwa moja masharti ya IMF ambayo kulingana na COTU yatasababishia wakenya mzigo zaidi wa ushuru.

Hali hiyo COTU inasema huenda ikasababisha maandamano ya kila mara ya wakenya ambao watakuwa wakilalamikia ugumu wa maisha kutokana na masharti hayo ya IMF.

Ushauri wa COTU kwa waziri Mbadi unajiri saa chache baada ya waziri huyo kukutana na wawakilishi wa shirika la fedha la kimataifa nchini kwenye afisi yake.

Atwoli anamshauri Mbadi kudurusu masharti ya IMF kwa makini na iwapo ataamua kuyatekeleza afanye hivyo kwa tahadhari kubwa akikumbuka athari zake kwa mwananchi wa kawaida.

Jambo lingine alilopendekeza Atwoli ni Kenya kujiepusha kabisa na shirika la IMF na wandani wake kabisa.

Website | + posts