Home Habari Kuu COTU yakejeli mipango ya waziri Kuria

COTU yakejeli mipango ya waziri Kuria

0

Muungano wa wafanyikazi nchini  COTU umetaja mipango ya waziri wa utumishi wa umma Moses Kuria, kusitisha makato ya wanachama wa vyama vya wafanyikazi na kufutilia mbali uajiri wa kudumu kuwa propaganda isiyo na mwelekeo.

Akizungumza na KBC naibu Katibu Mkuu wa COTU,Benson Okwaro, amesema vyama vya wafanyikazi vipo kwenye katiba na ni haki za kimsingi kila  mfanyikazi kujiunga na chama akipendacho.

Okwaro amesema pendekezo hilo kamwe halitafaulu kwani Kenya ni nchi ya Kidemokrasia na inayozingatia sheria na kuenda kinyume ni kuhujumu haki za wafanyikazi.

Okwaro ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama cha wafanyikazi wa sekta ya mawasiliano,COWU amesema pendekezo la waziri Kuria kuwaajiri wafanyikazi wote kwa kandarasi halitafaulu kwani litaigharimu serikali kiwango kikubwa cha pesa.

Katibu huyo pia amesisitiza kuwa  baadhi ya kazi haziruhusu uajiri wa kandarasi kwani zitahitilafiana na utendakazi.

Website | + posts