Home Michezo Copa America: wenyeji Marekani wabanduliwa

Copa America: wenyeji Marekani wabanduliwa

0
kra

Timu ya Marekani imeaga mashindano ya Copa America yanayoendelea nchini mwao baada ya kulazwa kwa bao moja mapema hii leo na viongozi wa kundi C Uruguay, hivyo kuambulia nambari tatu. Goli hilo lilitiwa wavuni na Mathías Olivera dakika ya 66.

Kwenye mechi nyingine ya kuhitimisha kundi hilo, Panama ilijikatia tiketi ya robo fainali ilipoilaza Bolivia mabao 3-1. Matatu hayo yalitingwa na José Fajardo, Eduardo Guerrero na César Yanis mnamo dakika za 22, 79 na 90+1 mtawalia. Moja la Bolivia lilifungwa na Bruno Miranda dakika ya 69.

kra

Mapema kesho Jumatano katika kundi D, Brazil watachuana na Colombia nao Costa Rica wamemyane na Paraguay.

Boniface Mutotsi
+ posts