Home Michezo Copa America: Argentina yaibandua Ecuador

Copa America: Argentina yaibandua Ecuador

0
kra

Mabingwa watetezi wa taji la bara la Amerika Argentina, wamefuzu kwa nusu fainali ya mashindano hayo kwa kuizaba Ecuador kupitia matuta ya 4-1.

Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida.

kra

Goli la Argentina lilifungwa na Lautaro Martínez nalo la Ecuador likapachikwa na Kevin Rodríguez dakika za 35 na 90+1 mtawalia.

Robo fainali ya pili itakuwa kati ya Venezuela na Canada hapo kesho saa kumi usiku.

Boniface Musotsi
+ posts