Jamhuri ya Demokrasia ya Congo inatarajia kupokea shehena ya kwanza ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Mpox ,Alhamisi Septemba 5 huku ya pili ikitarajiwa siku ya Jumamosi.
Congo imeshuhudia maambukizi makubwa ya ugonjwa wa Mpox barani Afrika huku shirika la Afya Duniani WHO, ikitangaza gonjwa hilo kuwa janga ulimwemguni mwezi uliopita na kuweka mikakati kabambe ya kuudhibiti.
Miji ya Washington na Brussels imeahidi kutoa msaada wa chanjo dhidi ya Mpox wakati taifa hilo likipanga kuwachanja raia wake kuanzia Septemba 8.
Zaidi ya watu 570 wamefariki kutokana na Mpox nchini Congo, na wengine zaidi ya 16,000 wakiambukizwa.