Home Kimataifa Cleophas Malala avuliwa wadhifa wa Katibu Mkuu wa UDA

Cleophas Malala avuliwa wadhifa wa Katibu Mkuu wa UDA

Baraza hilo lilisema liliandaa mkutano Ijumaa asubuhi, kufuatia ombi la wananchama waliotaka kujadili matukio yaliyokumba chama hicho hivi karibuni.

0
Cleophas Malala alivuliwa wadhifa wa Katibu Mkuu wa UDA.
kra

Chama cha United Democratic Alliance (UDA), kimebatilisha uteuzi wa Cleophas Malala kuwa kaimu Katibu Mkuu wake, na kumteua Hassan Omar kwa wadhifa huo.

Kulingana na taarifa kutocha chama hicho, Baraza Kuu la UDA NEC, limesema mabadiliko hayo yanatekelezwa mara moja.

kra

Baraza hilo lilisema liliandaa mkutano Ijumaa asubuhi, kufuatia ombi la wananchama waliotaka kujadili matukio yaliyokumba chama hicho hivi karibuni.

Aidha Baraza hilo Kuu pia liliangazia uchaguzi wa mashinani wa chama hicho, na kuagiza bodi ya kitaifa ya uchaguzi kuendelea na uchaguzi katika kaunti zilizosalia, kuambatana na mawasiliano ya hapo awali.

Kulingana na NEC, chaguzi hizo za nyanjani zitawezesha wanachama wa UDA kuwachagua viongozi wao kuanzia kiwango cha mashinani hadi kimataifa.

Mabadiliko hayo ya uongozi, yanajiri baada ya kushuhudiwa malumbano katika Makao Makuu ya chama hicho hivi majuzi.

Mnamo siku ya Jumatano, Joe Khalende akijitangaza yeye ndiye Katibu Mkuu wa chama hicho akidai kutimuliwa kwa Cleophas Malala katika wadhifa huo.

Baraza hilo liliezea wajibu wake wa kikatiba wa kutoa mwongozo za kisera na kisiasa kwa chama hicho, likisema linatekeleza wajibu muhimu kutekeleza ajenda za kisiasa za UDA.