Home Kaunti Chuo kikuu cha Masinde Muliro chazindua taaluma tatu mpya

Chuo kikuu cha Masinde Muliro chazindua taaluma tatu mpya

0

Chuo kikuu cha Masinde Muliro kimezindua taaluma tatu mpya kwa ushirika na mataifa ya Canada na Finland. Taaluma hizi ni sayansi ya daktari wa dharura itakayofunzwa kwa kiwango cha cheti na diploma na ambayo inafadhiliwa na nchi ya Canada, saikolojia ya neva na usalama wa viumbe zinazofadhiliwa na taifa la Finland.

Kwa mujibu wa kaimu naibu chansela wa chuo hicho Prof. Charles Mutahi, taaluma hizi zimeongeza idadi ya wanafunzi kutoka 22,000 hadi 24,000. Hadi sasa, wanafunzi 17 wa somo la daktari wa dharura wamesafiri nje ya nchi kwa mpango wa kubadilishana wanafunzi ,12 kati yao wakijiunga na shirika la msalaba mwekundu nchini Uingereza.

Akihiutubia wanahabari chuoni humo, Mutahi aliongeza kuwa chuo kimeekeza katika utafiti wa taaluma za sayansi, uhandisi,uchumi, usimamizi, dawa na sayansi ya jamii, jambo ambalo limevutia wafadhili kote duniani na kufanya chuo hicho kujulikana kote ulimwenguni.

Mwaka jana chuo hicho kilipokea shilingi milioni 100 kufanya utafiti wa funza. Mwaka huu, chuo hicho kimepokea ruzuku ya shilingi million 10 kutoka kwa hazina ya utafiti wa kitaifa na huenda kima hicho kikaongezeka kwani kuna wafadhili ambao wamevutiwa na mapendezo ya tafiti hizo na huenda wakafhadhili kwa shilingi milioni 10.

Zaidi ya hayo, alifichua kuwa idadi ya wanafunzi inazidi kuongezeka, hivyo wana mpango wa kujenga jumba kuu la somo la elimu litakalogarimu shilingi bilioni moja na lingine la sayansi ya afya litakojengwa kwenye shamba la ekari 34 walilomegewa na rais Ruto na ambalo hapo awali lilimilikiwa na shule ya kurekebishia tabia ya Kakamega,huku akirai serikali kusaidia kufadhili ujenzi huo.

Boniface Musotsi
+ posts