Home Habari Kuu Chuo kikuu cha Maasai Mara chafungwa kufuatia vurugumechi ya wanafunzi

Chuo kikuu cha Maasai Mara chafungwa kufuatia vurugumechi ya wanafunzi

0

Chuo kikuu cha Maasai Mara kilifungwa Alhamisi kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kuzua vurumai siku nzima, kwa madai ya usimamizi wa chuo kuhitilafiana na uchaguzi wa chama cha wanafunzi.

Kulingana na vyanzo vya taarifa hiyo wanafunzi walikerwa na hatua ya usimamizi wa shule kuingilia uchaguzi wao, wakidai usimamizi unapendekeza watu fulani kuchaguliwa ambao wataweza kuwathibiti.

Wanafunzi hao pia walijawa na hamaki baada ya kubaini kuwa bodi ya kusikiza rufaa za uchaguzi ilikuwa imehiari kuahirisha uchaguzi huo hadi wakati usiojulikana ndiposa wakaingia barabarani.

Baadaye naibu Chansela wa chuo hicho Professa Godrik Bulitia, alitoa arifa ya kutangaza kufungwa kwa chuo kwa wakati usiojulikana.

Website | + posts