Home AFCON 2023 Chui kuvaana na tembo huku Bafana wakipimana ubabe na tai nusu...

Chui kuvaana na tembo huku Bafana wakipimana ubabe na tai nusu fainali za AFCON

0

Makala ya 34 ya kindumbwendumbwe cha kombe la AFCON yatarejea Jumatano usiku tai wa Nigeria, wakicheza nusu fainali  ya kwanza dhidi ya Bafana bafana ya Afrika Kusini katika uwanja wa Bouake kaunzia saa mbili usiku.

Super Eagles watakuwa wakicheza nusu fainali kwa mara ya 15  na wakisawazisha rekodi ya Misri  kucheza nusu fainali mara nyingi zaidi.

Bafana Bafana watakuwa wakicheza nusu fainali kwa mara ya kwanza  baada ya miaka 24.

Afrika Kusini na Nigeria  watakutana kwa mara ya saba  mechi nne zikiishia sare ,huku kila mmoja akishinda mara moja.

Nigeria walimaliza wa pili kwa pointi saba kufuatia kushinda mechi mbili dhidi ya Guinea na Ivory Coast kabla ya kuilaza Cameroon mabao 2-0 katika awamu ya 16 bora na hatimaye kuibwaga Angola moja kavu katika robo fainali.

Afrika Kusini kwa upande wao walimaliza wa pili kundini E wakishindwa na Mali kabla ya kuwashinda Namibia na kutoka sare na Tunisia.

Bafana waliibandua Morocco mabao mawili kwa bila  katika raundi ya 16 bora na hatimaye kuilemea Cape Verde katika robo fainali.

Nusu fainali ya mwisho itakuwa kati ya wenyeji Ivory Coast ukipenda the Elephants dhidi ya Chui wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kuanzia saa tano usiku katika uchanjaa wa
Olympique Alassane Ouattara.

Tembo wa Ivory Coast walifuzu kwa mwondoano baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kundini A kwa alama 4 huku wakiibandua Senegal katika raundi ya 16 kupitia penati na hatimaye kuwalaza Mali 2-1 katika robo fainali.

DRC Walichukua nafasi ya pili katika kundi F wakitoka sare mechi zote tatu na kuwashinda Misri kupitia penati katika awamu ya 16 bora  na hatimaye kusajili ushindi wa kwanza ya kipute cha mwaka huu walipoishinda  Guinea mabao 3 -1.

Ivory Coast wameshinda mara sita nao DRC wakaibuka kidedea mechi nne huku michuano mitatu ikiishia sare.

Washindi watarejea uwanjani kwa fainali Jumapili wakati washinde wakimenyana kuwania nishani ya shaba.