Home Burudani Chipukeezy Show kuanza Septemba 11 kwenye runinga ya KBC

Chipukeezy Show kuanza Septemba 11 kwenye runinga ya KBC

0

Kipindi cha mahojiano na vichekesho kinachojulikana kama “Chipukeezy Show” kitaanza kupeperushwa na runinga ya kitaifa KBC Jumatatu Septemba 11, 2023. Kitakuwa Kikionyeshwa kila Jumatatu usiku kati ya saa mbili na saa tatu.

Mwanzilishi wa kipindi hicho mchekeshaji Vincent Mwasia maarufu kama Chipukeezy alisema dhamira ya kipindi hicho ni kutoa jukwaa kwa talanta ibuka ambapo zinaweza kukuzwa na kuhakikisha zinawapa mapato.

Alizungumza wakati wa kutia saini makubaliano na kaimu mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji nchini KBC Bwana Samuel Maina.

Kipindi hicho kitanakiliwa katika maeneo tofauti ya jiji la Nairobi na baadaye kitanakiliwa katika sehemu nyingine nchini.

Bwana Maina alihimiza vijana wawe wakiwezesha wenzao kila wanapopata fursa hasa wakati huu ambapo nchi inakabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Wakati wa kutangaza marejeo ya onyesho hilo lake mwezi Agostim Chipukeezy alionekana kujawa na furaha kurejelea kipindi hicho baada ya mapumziko ya miaka mitatu.

Alishukuru Mungu kwa mibaraka na mashabiki wake kwa uvumilivu.

Chipukeezy alisifia runinga ya KBC Channel 1 makao mapya ya Chipukeezy Show akiitaja kuwa runinga iliyo rahisi kutazama.

Huwa anashirikiana na mchekeshaji mwenza Kartelo katika kuongoza kipindi hicho.

Website | + posts