Home Biashara China yaahidi msaada wa dola bilioni 51 kwa mataifa...

China yaahidi msaada wa dola bilioni 51 kwa mataifa ya Afrika

0
kra

Uchina imeahidi kutoa msaada wa dola za Kimarekani bilioni 51 kufadhili miradi 30 ya miundo msingi barani Afrika, inayokisiwa kubuni nafasi za ajira milioni moja.

Rais wa Uchina Xi Jinping alifichua hayo wakati wa kongamano la China na mataifa ya Afrika .

kra

Xi Jinping aliongeza kuwa Uchina inalenga kupanua soko lake kwa mataifa yote 50 ya Afrika yalihudhuria kongamano hilo.

Kulingana na taarifa hiyo Uchina itatoa bilioni dola 50 za Kimarekani kufadhili miradi ya miundo mbinu barani Afrika, huku kiwango kingine cha dola bilioni 210 zikitolewa kama mikopo.

Uchina pia imekariri kujitolea kuanzisha miradi 30 ya kawi safi barani Afrika, katika jitihada za kupunguza uhaba wa umeme ambao umeathiri ukuaji wa viwanda afrika.

Website | + posts