Home Habari Kuu China na Urusi zafanya doria ya kwanza ya pamoja ya ndege za...

China na Urusi zafanya doria ya kwanza ya pamoja ya ndege za mashambulizi karibu na Marekani

0
kra

Urusi na China zimefanya doria ya pamoja katika Bahari ya Pasifiki ya kaskazini na Bahari ya Bering karibu na pwani ya Alaska.

Nchi hizo mbili zimefanya doria kadhaa za pamoja hapo awali, na Urusi mara kwa mara hupeleka ndege zake za mashambulizi kwenye Bahari ya Bering.

kra

Lakini doria ya pamoja ya Jumatano ilikuwa ya kwanza iliyojumuisha ndege za mashambulizi kutoka nchi zote mbili katika eneo la kaskazini mwa Pasifiki.

Urusi na China zilisema “hazikulenga mtu wa tatu”, huku kituo cha pamoja cha ulinzi wa anga cha Marekani na Canada (NORAD) kikisema ndege za mashambulizi ambazo kilizizuia zilikaa katika anga ya kimataifa na “hazikuonekana kama tishio”.

Lakini Seneta wa Alaska Lisa Murkowski alielezea tukio hilo kama “uchochezi ambao haujawahi kufanywa na wapinzani wetu”, na kuongeza kuwa “ilikuwa mara ya kwanza kuzuiwa kufanya kazi pamoja.”

China imesema doria hiyo “haina uhusiano wowote na hali ya sasa ya kimataifa na kikanda”.

BBC
+ posts