Home Kimataifa China ina matarajio mazuri ya ukuaji wa kiuchumi licha ya kupoteza nafasi...

China ina matarajio mazuri ya ukuaji wa kiuchumi licha ya kupoteza nafasi yake kama nchi yenye idadi kubwa ya watu duniani

0

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), limesema kuwa idadi ya watu nchini India itakapofika katikati ya mwaka huu, inakadiriwa kuwa bilioni 1.4286, na kuifanya India kuwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani.

Kwa mara ya kwanza, mwaka jana, China ilirekodi ukuaji hasi wa idadi ya watu kwa karibu miaka 61 iliyopita.

Swali ni kwamba, kupoteza hadhi ya kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu kuna maana gani kwa China? Ongezeko hasi la idadi ya watu litaleta changamoto gani mpya katika uchumi wa China?.

Mtaalamu mwandamizi katika Jopo la kitaifa la Washauri bingwa katika Akademia ya Sayansi ya Jamii nchini China, Cai Fang anasema hakuna haja ya kuwa na wasiwasi wowote, na kwamba ongezeko hasi la idadi ya watu halibadili matarajio kuwa China itakuwa nchi kubwa kiuchumi duniani.

Mtaalamu huyo anasema, Mfuko wa Kimataifa wa Fedha (IMF) unakadiria kuwa, kutengana kwa China na Marekani kunaweza kusababisha hasara ya hadi asilimia 2 ya pato la dunia, ambalo litaathiri nchi nyingine duniani.

Anasema kadri hatua kali zaidi zinavyochukuliwa kupendelea nchi moja, ndivyo hasara kubwa itakavyokuwa, na muda si mrefu, nchi nyingine duniani zitafanya uamuzi utakaoendana zaidi na maslahi yao, kuliko kushawishiwa na nchi nyingine.

Kama mwenza mkubwa wa Marekani, Ulaya imetafakari upya matokeo yasiyotarajiwa ya kufuata uongozi wa Marekani, na wengi wameeleza utayari wao wa kukwepa Vita Baridi na “utengano.”

Pia kundi la BRICS, ASEAN, Latin America, Afrika, na Mashariki ya Kati, na maeneo pamoja mashirika ya kikanda vimeonyesha nia hii ya kukwepa kuchagua upande wowote, na kufanya inavyotakiwa katika ushirikiano kati yao na China.

Akizungumzia hoja hii, Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii na Uchumi kati ya Afrika na China kutoka Tanzania Profesa Humphrey Moshi amesema, kuna mambo manne ambayo yanapaswa kufanyiwa tathmini kuhusu suala la ongezeko la idadi ya watu.

Amesema jambo la kwanza, ni kwamba idadi ya watu inapaswa kuendana na kiwango cha maendeleo ya uzalishaji wa nchi moja, na kwamba idadi kubwa ya watu inaweza kuwa mzigo.

Jambo lingine alilolisema ni mfumo wa ongezeko hilo, ikimaanisha idadi ya wazee na vijana.

Kama katika nchi kuna idadi kubwa ya wazee kuliko vijana, maendeleo hayawezi kupatikana kwa urahisi, lakini kama idadi kubwa ya watu ni vijana, itakuwa ni neema, kwa kuwa vijana, tena wenye ajira, ni nguvukazi muhimu katika nchi husika.

Profesa Moshi amesema, kitu kingine kinachopaswa kufuatiliwa ni kiwango cha elimu, utaalamu na teknolojia kwa jamii husika.

Amesema kama kiwango hicho kikiwa ni kikubwa, kitakuwa ni kichocheo kikubwa katika kuleta maendeleo ya haraka na kupunguza umasikini, jambo ambalo China imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Jambo la mwisho la kutazama ni umri wa kuishi, ambao utawafanya watu wenye uwezo wa kufanya kazi, kufanya kazi kwa muda mrefu kabla ya kustaafu.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here