Home Michezo Cheptegei kuongoza Uganda kwa mashindano ya riadha duniani mjini Budapest

Cheptegei kuongoza Uganda kwa mashindano ya riadha duniani mjini Budapest

Katika makala ya mwaka jana mjini Oregon Marekani,Uganda iliwakilishwa na wanariadha 17 huku ikizoa dhahabu moja ,fedha 1 na shaba moja .

0

Bingwa mtetezi wa dunia katika mita 10,000 Joshua Cheptegei, bingwa wa Jumuiya ya Madola katika mita 5,000 na 10,000 Jacob Kiplimo na bingwa wa dunia katika mita 800 mwaka 2019 Halima Nakaayi, ni miongoni mwa wanariadha walioteuliwa kuiwakilisha Uganda kwa makala ya 19 ya mashindano ya riadha ulimwenguni yatakayoandaliwa mjini Budapest nchini Hungary kati ya Agosti 19 na 27 mwaka huu.

Kiplimo na Cheptegei watashiriki fani za mita 5,000 na mita 10,000 huku pia Sarah Chelangat akitimka fani za mita 5,000 na mita 10,000.

Shirikisho la riadha nchini Uganda lilitaja orodha ya wanariadha 22 watakaoshiriki mashindano hayo mapema wiki hii.

Wanariadha wengine waliojumuishwa katika timu hiyo ya Uganda ni bingwa wa Olimpiki katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji Peruth Jemutai na mshindi wa nishani ya shaba ya dunia katika mita 5,000 mwaka 2022 Oscar Chelimo.

Hiki ndicho kikosi kamili cha Uganda kwa mashindano ya riadha ulimwenguni
Wanaume
200m – Tarsis Orogot
800m – Tom Dradiga
3000m SC – Leonard Chemutai
5000m – Joshua Cheptegei, Jacob Kiplimo, Oscar Chelimo
10,000 – Joshua Cheptegei, Jacob Kiplimo, Rogers Kibet, Joel Ayeko
Marathon – Andrew Rotich Kwemoi, Victor Kiplangat, Stephen Kissa

Wanawake
800m – Halimah Nakaayi
1500m – Janat Chemusto, Winnie Nanyondo
3000m SC – Peruth Chemutai
5000m – Sarah Chelangat
10,000m – Sarah Chelangat, Stella Chesang
Marathon – Rebecca Cheptegei, Doreen Chesang, Mercyline Chelangat.

Katika makala ya mwaka jana mjini Oregon nchini Marekani, Uganda iliwakilishwa na wanariadha 17 huku ikizoa dhahabu moja, fedha 1 na shaba moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here