Home Kimataifa Chepkoech na Cherotich wafuzu kwa fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi

Chepkoech na Cherotich wafuzu kwa fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi

0
kra

Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji Beatrice Chepkoech na mshindi wa nishani ya shaba ya dunia Faith Cherotich, wamejikatia tiketi kwa fainali ya Olimpiki  Jijini Paris Ufaransa mapema Jumapili.

Cherotich alimaliza wa pili katika mchujo wa kwanza akitumia muda wa dakika 9 sekunde 10.57,nyuma ya bingwa mtetezi Peruth Chemutai wa Uganda aliyetimka kwa dakika 9 sekunde 10.51 .

kra
Faith Cherotich akishiriki mchujo wa mita 3,000 kuruka viunzi na maji jijini Paris,Ufaransa picha hisani/Kelly Ayodi

Chepkoech ameongoza mchujo wa tatu akitumia dakika 9 sekunde 13.56.

Hata hivyo bingwa wa Jumuiya ya Madola Jackline Chepkoech alikosa kufuzu, baada ya kumaliza wa mwisho katika mchujo wa pili ulioshindwa na bingwa wa dunia Winfred Mutile wa Bahrain .

Fainali ya shindano hilo ambalo Kenya inawinda dhahabu ya kwanza tangu mwaka 2008 lilipojumuishwa katika Olimpiki kwa wanawake,itaandaliwa Jumanne Agosti 6.

Website | + posts