Home Michezo Chebet na Obiri kushiriki New York City Marathon

Chebet na Obiri kushiriki New York City Marathon

Chebet alitwa taji hiyo mwaka jana akishiriki kwa mara ya kwanza kwa muda wa saa 2 dakika na sekunde 41, ikiwa miezi 11 pekee baada ya kushinda Boston Marathon.

0

Bingwa mtetezi wa New York City Marathon Evans Chebet atakabiliana na Geoffrey Kamworor katika makala ya mwaka huu yatakayoandaliwa Novemba 5, mwaka huu.

Chebet alitwa taji hiyo mwaka jana akishiriki kwa mara ya kwanza kwa muda wa saa 2 dakika na sekunde 41, ikiwa miezi 11 pekee baada ya kushinda Boston Marathon.

Kamworor, ambaye ni bingwa mara tatu wa nusu marathon duniani, atakuwa akiwania taji hiyo kwa mara ya nne baada ya kutawazwa bingwa mwaka 2017 na 2019.

Bingwa wa mwaka 2021 Albert Korir na mwanariadha wa Marekani mzawa wa Kenya Edward Cheserek atashiriki kwa mara ya kwanza.

Sharon Lokedi atarejea Marekani kutetea taji yake dhidi ya bingwa wa New York Half Marathon na Boston Marathon Hellen Obiri, bingwa mtetezi wa Olimpiki Peres Jepchirchir na mshikilizi wa rekodi ya dunia Brigid Kosgei watashiriki.

Wakenya wengine watakaoshiriki ni bingwa mara mbili wa dunia Edna Kiplagat na Viola Kibiwott pia watarejea.