Bingwa mara mbili wa Olimpiki Beatrice Chebet na bingwa wa Dunia Mary Moraa, waliibuka mabingwa katika mkondo wa 14 wa Zurich Diamond League Alhamisi usiku.
Chebet alishinda mbio za mita 5,000 akisajili muda wa kasi duniani wa dakika 14 sekunde 9.52 .
Wahabeshi Eljagayehu Taye na Tsigie Gebreselama walimaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia.
Moraa alitoka nyuma latika mzunguko wa mwisho na kutwaa ushindi kwa dakika 1 sekunde 57.08.
Mwingereza Georgia Bell na Mmarekani Addison Willey walichukua nfasi za pili na tatu katika usanjari huo.
Wakenya Jacob Krop na Cornelius Kimboi wakimalIa nafasi za kwanza na pili mtawalia katika mita 3,000, huku Isaac Kimeli wa Ubelgiji akiambulia nafasi ya tatu.
Reynold Cheruiyot na Timothy Cheruiyot walichukua nafasi za 6 na 11 katika mita 1500.
Yared Nuguse wa Marekani aliongoza akifuatwa na Yakub Ingebrigsten wa Norway.