Home Michezo Chebet awika Oslo na kuvunja rekodi ya miaka 24

Chebet awika Oslo na kuvunja rekodi ya miaka 24

0

Mshindi wa nishani ya fedha ya dunia Beatrice Chebet, aliandikisha rekodi mpya ya mita 3000 ya mashindano ya Oslo Diamond League maarufu kama Bislet Games, yaliyoandaliwa nchini Norway Alhamisi usiku.

Chebet ambaye pia ni bingwa wa Jumuiya ya Madola, aliziparakasa mbio hizo za mizunguko saba unusu kwa kutumia dakika 8 sekunde 25 nukta 01, ukiwa muda wa kasi ulimwenguni na pia muda bora wa kibinafsi alivunja rekodi iliyosimama kwa miaka 24 katika mashindano hayo.

Wakenya walitala mbio hizo wakitwaa nafasi tatu bora Lillian Kasait akimaliza wa pili kwa dakika 8 sekunde 25 nukta 90 huku Margaret Chelimo, akiambulia nafasi ya tatu akifika utepeni kwa dakika 8 sekunde 26 nukta 14.

Timothy Cheruiyot aliridhia nafasi ya nne katika mita 1500 akitumia dakika 3 sekunde 28 nukta 08.

Yakub Ingebrigtsen wa Norway alitwaa ubingwa akisajili rekodi mpya ya mashindano ya dakika 3 sekunde 27 nukta 25,akifuatwa na Mohammed Katir kutoka Uhispania kwa dakika 3 sekunde 28 nukta 98.

Wahabeshi walitawala mbio za mita 5,000 wakiongozwa na Yomif Kejelcha aliyetimka kwa dakika 12 sekunde 41 nukta 74,akifuatwa na Jacob Kiplimo wa Uganda kwa dakika 12 sekunde 41 nukta73.

Marie -Josée Talou wa Ivory Coast alisajili ushindi wa kwanza alipofyatuka mita 100 kwa sekunde 10 nukta 75 ukiwa muda wa kasi ulimwenguni.

Strachan Anthonique wa Bahamas alichukua nafasi ya pili kwa sekunde 10 nujta 92,  huku bingwa wa dunia katika mita 200 Shericka Jackson wa Jamaica, akichukua nafasi ya tatu kwa sekunde 10 nukta 98

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here