Home Kimataifa Chebet avunja nuksi ya Olimpiki kwa vipusa wa Kenya mita 10,000

Chebet avunja nuksi ya Olimpiki kwa vipusa wa Kenya mita 10,000

0
kra

Beatrice Chebet alipeperusha bendera ya Kenya kwa njia ya kipekee Ijumaa usiku ugani Stade De  France, baada ya kutwaa dhahabu ya mbio za mita 10,000.

Dhahabu hiyo ambayo aliinyakua kwa kutumia dakika 30 sekunde 43.25 , ilikuwa yake ya pili katika Olimpiki ya Paris, baada ya kuzoa ile ya mita 5,000.

kra

Chebet aliye na umri wa miaka 24 ameingia kwenye madaftari ya historia kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Kenya, kutwaa ubingwa wa Olimpiki katika mita 10,000.

Mshikilizi huyo wa rekodi ya dunia aliyosajili mwezi Juni mwaka huu alijizatiti katika  mita 100 za mwisho, na kumbwaga Mwitaliano Nadia Batocletta aliyemaliza wa pili, huku Sifan Hassan wa Uholanzi akiridhia nishani ya shaba.

Matokeo hayo yanaikweza Kenya hadi nafasi ya 25 kwa nishani 6,dhahabu 2 fedha 1 na shaba 3.

Chebet ameshinda dhahabu za mita 5,000 na 10,000 akijitangaza kuwa malkia wa mbio za masafa marefu, naye  bingwa mtetezi wa mita 1,500 Faith Kipyegon akiwa mshindi wa medali ya pekee ya  fedha mita 5,000.

Shaba tatu za Kenya zimeshindwa kupitia kwa Faith Cherotich mita 3,000 kuruka viunzi na maji,Mary Moraa mita 800 na Abraham Kibiwot pia mita 3,000 kuruka viunzi na maji .

 

Website | + posts