Home Kimataifa Olimpiki ya Paris: Chebet atwaa dhahabu, Kipyegon fedha na Moraa shaba

Olimpiki ya Paris: Chebet atwaa dhahabu, Kipyegon fedha na Moraa shaba

Kenya sasa ni 31 kwenye msimamo wa nishani, kwa dhahabu 1 fedha 1 na shaba 1.

0
kra

Beatrice Chebet alishinda dhahabu ya kwanza  ya Kenya  katika michezo ya Olimpiki ya Paris, katika fainali ya mita 5,000 Jumatatu usiku.

Chebet aliziparakasa mbio hizo kwa dakika 14 sekunde 28.56.

kra

Faith Kipyegon alishinda fedha kwa dakika 14 sekunde 29.60, huku shaba ikimwendea Sifan Hassan wa Uholanzi.

Awali, kulikuwa na kiroja baada ya Kipyegon kupokonywa medali ya fedha kwa kisingizio cha kumsukuma Gudaf Tsegay wa Ethiopia.

Baada ya maafisa wa Kenya kukata rufaa, Kipyegon alirejeshewa medali yake ya fedha.

Dhahabu ya Chebet ilikuwa ya pili  kwa Kenya katika Olimpiki tangu Vivian Cheruiyot, aibuke bingwa mwaka 2016 mjini Rio De Janeiro.

Mary Moraa aliongeza nishani ya shaba kwa Kenya katika mita 800 akitumia dakika 1 sekunde 57.42.

Keely Hodgkinson wa Uingereza alishinda dhahabu kwa dakika  1 sekunde 56.72, wakati Tsiye Duguma wa Ethiopia akishinda fedha.

Kenya sasa inaorodheshwa ya 31 kwenye msimamo wa nishani kwa dhahabu 1 fedha 1 na shaba 1.

Matokeo hayo yana maana kuwa Kenya haijashinda dhahabu ya mita 800 ya Olimpiki, tangu Pamela Jelimo ashinde dhahabu ya kwanza mwaka 2008.

Website | + posts