Home Habari Kuu Chebet atwaa dhahabu na kuweka rekodi ya kilomita 5 mjini Riga

Chebet atwaa dhahabu na kuweka rekodi ya kilomita 5 mjini Riga

0

Bingwa wa dunia wa mbio za nyika Beatrice Chebet, ametwaa dhahabu ya  kilomita 5 katika makala ya kwanza ya  mashindano ya dunia ya mbio za barabarani, akiweka rekodi mpya ya dakika 14 na sekunde 35 .

Mashindano hayo yameandaliwa Jumapili mjini Riga nchini Latvia huku Chebet ambaye pia ni mshindi wa nishani ya fedha  ya dunia  katika mita 5,000 mwaka huu, akitwaa uongozi katika kilomita ya  4 na kukata utepe wa kwanza.

Lillian Kasait Rengeruk wa Kenya ameshinda medali ya fedha  kwa muda wa dakika 14 na sekunde 39, huku  Elgayehu Taye wa Ethiopia aliyekuwa akiongoza kutoka mwanzo akiridhia nsihani ya shaba.