Home Michezo Chebet atawazwa bingwa wa nyika mwaka 2023/2024

Chebet atawazwa bingwa wa nyika mwaka 2023/2024

0
kra

Beatrice Chebet ndiye bingwa wa msimu wa mwaka 2023/2024 wa msururu wa mbio za nyika ulimwenguni, baada ya kuhifadhi taji ya dunia wiki iliyopita nchini Serbia.

Kulingana na msusruru huo, wanariadha huorodheswa kulingana na matokeo yao katika mbio tatu bora  kati ya mwezi Septemba mwaka 2023 na Machi 31 mwaka huu.

kra

Chebet aliibuka mshindi wa msimu baada ya kusajili ushindi wa mbio za Atapuerca mwezi Oktoba mwaka uliopita na baadaye kutwaa ushindi katika mbio za Elgoibar mwezi Februari mwaka huu na kisha kuhifadhi taji ya dunia wiki iliyopita.

Kwa jumla, Chebet alizoa pointi 3880 na atapokea zawadi ya yuro 10,000.

Edinah Jebitok alimaliza wa pili baada ya kushinda mbio za   Seville, Venta de Banos na Hannut.

Rodrique Kwizera kutoka Burundi alitawazwa mshindi wa msimu kwa wanaume akizoa alama 3700 huku Mkenya Ronald Kwemoi akimaliza wa tatu kwa pointi 3610.

Website | + posts