Home Habari Kuu Chama cha ODM chataka kutekelezwa kwa ripoti ya NADCO

Chama cha ODM chataka kutekelezwa kwa ripoti ya NADCO

Viongozi wa ODM walisema serikali haijamakinika kutekeleza ripoti hiyo,  wakitaja hali hiyo kuwa tishio kwa udhabiti wa taifa.

0
Viongozi wa chama cha ODM wataka kutekelezwa kwa ripoti ya kamati ya NADCO.

Viongozi wa chama cha Orange Democratic Movement ODM, kutoka kaunti ya Siaya wametoa wito wa kutekelezwa kikamlifu kwa ripoti ya kamati ya maridhiano ya kitaifa (NADCO), katika muda uliowekwa.

Wakiongozwa na Gavana wa kaunti ya Siaya James Orengo, viongozi hao walisema serikali haijamakinika kutekeleza ripoti hiyo,  wakitaja hali hiyo kuwa tishio kwa udhabiti wa taifa.

Akizungumza wakati wa mkutano wa wajumbe wa chama cha ODM kutoka kaunti ya Siaya, Orengo alisema muungano wa Azimio hautakuwa na lingine ila kurejea kwa wananchi ikiwa serikali ya Kenya kwanza haitajukumika kutekeleza ripoti hiyo.

Wakati huo huo, Gavana huyo alisema hakuna pengo katika uongozi wa chama cha ODM, huku akipuzilia mbali siasa za uridhi chamani.

Orengo, aliyesoma maazimio ya mkutano huo, alisema chama hicho kinamuunga mkono kikamilifu waziri mkuu wa zamani Raila Odinga huku wajumbe wa chama hicho wakiazimia kuimarisha juhudi za kuwasajili wanachama wapya.

Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Seneta wa Siaya Dkt. Oburu Oginga, mwakilishi mwanamke wa kaunti hiyo Dkt. Christine Ombaka, wabunge  Opiyo Wandayi (Ugunja), Otiende Amollo (Rarieda) na Samuel Atandi (Alego/Usonga)

Website | + posts