Home Michezo CAF yatangaza droo ya mchujo kufuzu AFCON 2025

CAF yatangaza droo ya mchujo kufuzu AFCON 2025

0

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetangaza ratiba ya mechi za mchujo kufuzu kwa fainali za kombe la bara Afrika AFCON mwaka 2025 nchini Morocco.

Kulingana na droo hiyo iliyoandaliwa Jumatano jijini Cairo Misri,mataifa manane yaliyo katika nafasi za mwisho katika msimamo wa dunia wa FIFA, yatapambana kwa mikondo miwili huku washindi wanne wakijumuishwa katika droo ya makundi itakayoshirikisha nchini 48.

Somalia itapambana na Eswatini nao Sudan Kusini waanzie ugenini dhidi ya Sao Tome,wakati Chad wakikwangurana na Mauritius kisha Djibouti wamalize udhia na Liberia.

Michuano hiyo itasakatwa katika dirisha la mechi za kimataifa kati ya tarehe 20 na 26 mwezi ujao.

Website | + posts