Home Habari Kuu CAF yaongeza donge la pesa kwa washindi wa AFCON

CAF yaongeza donge la pesa kwa washindi wa AFCON

0
CAF President Patrice Motsepe during the African Clubs Association General Assembly held at Marriott Mena House in Cairo, Egypt on 30 November 2023 ©Weam Mostafa/BackpagePix

Shirikisho la soka barani Afrika, CAF limeongeza kitita cha zawadi ya pesa kitakachotuzwa washindi wa mwaka huu wa kombe la AFCON.

CAF imeongeza kiwango cha fedha hizo kwa asilimia 40 ambapo mshindi atapokea shilingi bilioni 1.1, huku timu ya pili ikitia kibindoni shilingi milioni 632.

Timu zitakazofika nusu fainali zitatuzwa shilingi 396.

Kipute cha mwaka huu kitaanza rasmi tarehe 13 mwezi huu hadi Februari 11 nchini Ivory Coast.

Website | + posts