Home Kaunti Bweni lateketea shule ya upili ya wavulana ya Shanderema

Bweni lateketea shule ya upili ya wavulana ya Shanderema

0
Bweni moja limeteketea katika shule ya upili ya wavulana ya Shanderema katika eneo bunge la Shinyalu, kaunti ya Kakamega.
Kisa hicho kiliwalazimu wanafunzi zaidi ya 70 kustahimili makali ya baridi kali usiku kucha.
Kulinga na wakazi wakiongozwa na mmoja wa wafadhili wa shule hiyo Eric Lung’aho, the moto huo ulizuka jioni na kusambaa kwa kasi ukiharibu mali yote ya wanafunzi.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Simon Wazenga amesema moto huo ulizuka wakati wanafunzi wakiwa darasani.
Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha moto huo.
Carolyn Necheza
+ posts