Home Burudani Butita amshukuru Rais Ruto kwa fursa

Butita amshukuru Rais Ruto kwa fursa

0

Mchekeshaji na mbunifu Eddie Butita amemshukuru Rais William Ruto kwa kumtunukia fursa ya kuandamana naye katika ziara yake ya Marekani.

Butita alichapisha picha kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii akisema anaondoka kuelekea Marekani leo kwa ajili ya kumzindikisha Rais kwenye ziara hiyo.

Alisema uhusika wake kwenye ziara hiyo ni ishara tosha kwamba wabunifu wataangaziwa kwenye mazungumzo yatakayofanyika wakati wa ziara hiyo ya Marekani ambapo watakutana na Rais Joe Biden.

Ziara hiyo inatarajiwa kuanza rasmi Mei 23, 2024 na Rais Ruto anatizamia kukutana na wadau muhimu katika sekta ya ubunifu na burudani ili kutafuta njia ya kushirikiana na hatimaye kuboresha uchumi wa ubinifu humu nchini.