Home Kimataifa Burundi yafunga mipaka yake na Rwanda

Burundi yafunga mipaka yake na Rwanda

Haijabainika mara moja ikiwa kufungwa kwa mpaka ni pamoja na ardhi na anga.

0

Burundi imefunga mipaka yake na Rwanda baada ya kuishtumu jirani yake kufadhili mashambulizi ya waasi.

Disemba mwaka jana Red Tabara, kundi la waasi wa Burundi, liliua watu 20 karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Rais wa Rwanda Paul Kagame anakanusha madai hayo, lakini serikali ya Burundi imemtaja kuwa “jirani mbaya”.

“Tumesitisha uhusiano naye hadi abadilike” alisema Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi Martin Niteretse.

Rais wa Burundi √Čvariste Ndayishimiye alitoa shutuma hizo mwezi Disemba kufuatia shambulio hilo.

Serikali ya Rwanda ilijibu kwamba “inajutia kufungwa kwa mpaka na Burundi kwa upande mmoja”, kulingana na AFP.

Ilisema kufungwa kwa mpaka ni “uamuzi wa bahati mbaya” ambao unakiuka kanuni za ushirikiano wa kikanda na ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Red Tabara alikiri kutekeleza shambulio hilo la Desemba, lakini ilisema ilikuwa imewaua wanajeshi tisa na afisa mmoja wa polisi.

Kundi hilo linafanya kazi kutoka jimbo la Kivu Kusini nchini DR Congo linalopakana na Burundi.

Haijabainika mara moja ikiwa kufungwa kwa mpaka ni pamoja na ardhi na anga.

Mwaka 2015 Burundi ilifunga mpaka wake na Rwanda kutokana na mivutano ya kisiasa na kisha kwa sababu ya Covid-19.Miaka saba baadaye mipaka ilifunguliwa tena.

Wakati huo ni njia za kuvuka ardhi pekee ndizo zilizoruhusiwa.Lakini shirika la ndege la RwandAir halikusimamisha safari zake za kibiashara kuelekea Burundi.

Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi umekuwa wa kusuasua licha ya mambo mengi yanayofanana kati ya mataifa hay ikiwemo lugha muundo wa kikabila na historia ya ukoloni.

Website | + posts
BBC
+ posts