Home Habari Kuu Buriani ya marehemu Kimeu kuandaliwa Matuu Jumamosi

Buriani ya marehemu Kimeu kuandaliwa Matuu Jumamosi

0

Aliyekuwa mtangazaji nguli wa michezo katika Shirika la Utangazaji nchini KBC,atapumzishwa Jumamosi nyumbani kwake Matuu kaunti ya Machakos.

Kimeu alikuwa amefanya kazi katika shirika la KBC kati ya mwaka 1989 hadi alipostaafu mwaka 2022.

Marehemu Peter Kimeu akiwa katika maadhi todauti

Ustadh Peter Kimeu alikuwa akipeperusha vipindi vya michezo katika Idhaa ya Taifa enzi hizo, vikiwemo Ulimwengu wa Michezo,Ukumbi wa Spoti na Mwengo wa Spoti .

Katika amali yake aliwalea na kuwakuza watangazaji maarufu nchini.

Kimeu alifariki Jumapili iliyopita baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mwenda zake Kimeu alizaliwa mwaka 1962 katika kijiji cha Mumina eneo la Yatta kaunti ya Machakos, na amemuacha mjane na wana wa kiume wawili.

Buriani Ustadh.