Home Kimataifa Bunge latilia shaka uwezo wa Safaricom kusimamia mfumo wa teknolojia...

Bunge latilia shaka uwezo wa Safaricom kusimamia mfumo wa teknolojia ya afya (IHTS)

0
kra

Wabunge wametilia shaka mchakato wa wizara ya afya kutoa tenda kwa kamouni ya Safaricom kusimamia mfumo wa teknolojia ya afya kwa wote (IHTS).

Kandarasi hiyo ya kima cha shilingi bilioni 104.8 kwa kipindi cha miaka 12 ilipewa kampuni ya Safaricom.

kra

Safaricom inatarajiwa kununua na kuweka mfumo wa kidijitali wa afya .

Hata hivyo wambunge wamekosa hatua hiyo wakisema Safaricom inalimiliki asimilia 13 pekee ya huku mshirika wake kampuni ya Apiero waliyopewa pamoja kandarasi ikimiliki zaidi ya asilimia 50.

Mwenyekiti wa kamati ya afya katika bunge la kitaifa Dkt Robert Pukose amesema huenda Kampuni ya Apiero Limited, ambayo haina ujuzi ikashindwa kutoa huduma bora katika mfumi huo mkubwa wa afya kwani bado inafanya majaribio.

Pukuse amemwagiza Waziri wa afya na Katibu wake kufika mbele ya kamati Jumatatu Septemba 30, kujibu maswali kuhusu sababu za kutoa zabuni hiyo kwa Safaricom.

Pukuse pia amehoji ni sababu za wizara ya afya kutafuta mfumo mpya wa teknolojia ya mawasiliano katika wizara ya afya badala ya kutumia mfumo uliokuwepo wa NHIF.

Website | + posts