Home Kimataifa Bunge la Kitaifa laidhinisha kutumwa kwa polisi 1,000 Haiti

Bunge la Kitaifa laidhinisha kutumwa kwa polisi 1,000 Haiti

0
kra

Bunge la Kitaifa limeidhinisha pendekezo la serikali ya Kenya la kutuma maafisa wa polisi 1,000 kushika doria nchini Haiti.

Bunge hilo lilipiga kura kwenye kikao cha leo Alhamisi asubuhi na kuidhinisha pendekezo hilo ambalo sasa litawasilishwa kwa bunge la Seneti ili pia kutafuta idhini yake.

kra

Ikiwa pia litaidhiniwa na Seneti, uidhinishaji huo utatoa fursa kwa serikali kuwatuma polisi hao wa Kenya nchini Haiti.

Hata hivyo, serikali italazimika kusubiri uamuzi wa kesi ya kiongozi wa chama cha Third Way Alliance EKuru Aukot iliyopinga pendekezo hilo.

Mahakama kuu ilisitisha shughuli hiyo kusubiri kuamuliwa kwa kesi hiyo.

Website | + posts