Home Habari Kuu Bunge la Ufaransa kukosa chama kimoja kikuu

Bunge la Ufaransa kukosa chama kimoja kikuu

0
kra

Ufaransa itakuwa na bunge ambalo halina chama kimoja kikuu kufuatia uchaguzi wa Jumapili ambapo chama cha mrengo wa kulia RN kilikosa kupata wingi wa viti bungeni.

Matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha ushindi mkubwa wa muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto NFP, huku chama cha Rais Emmanuel Macron centrist Ensemble alliance kikiwa nambari mbili na RN nambari tatu.

kra

Inasubiriwa kuona jinsi bunge la taifa hilo litaendesha shughuli zake kwani makundi hayo matatu hayajawahi kushirikiana kisiasa.

Jana ilikuwa awamu ya pili ya uchaguzi wa ubunge ulioandaliwa mapema na Rais Macron na ambao aliutangaza mwezi mmoja uliopita.

Baada ya muungano wa RN kufanya vyema kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi huo wiki moja iliyopita, wawaniaji wa mirengo ya kulia na kati walijiondoa.

Hatua hiyo inachukuliwa kuwa ya kimkakati kwa lengo la kufanya wafuasi wao kuunga mkono mwaniaji mmoja.

Wataalamu wa masuala ya siasa nchini Ufaransa wanahisi kwamba uchaguzi huo ambao Macron aliandaa mwenyewe umesababisha awe kiongozi hafifu ambaye hana wingi wa viti bungeni.

Ushawishi wake kimataifa pia huenda ukapungua kufuatia matokeo ya uchaguzi huu wa ubunge. Hatua yake ya kuandaa uchaguzi huo mapema inaaminika kuchochewa na matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa bunge la muungano wa Ulaya.