Home Kimataifa Bunge la Marekani laiwekea ICC vikwazo

Bunge la Marekani laiwekea ICC vikwazo

0

Bunge la Wawakilishi la Marekani limepiga kura kupitisha sheria ambayo itaiwekea vikwazo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) baada ya mwendesha mashtaka wake kuomba hati ya kukamatwa kwa maafisa wa Israel.

Hatua hiyo imekuja baada ya mwendesha mashtaka wa mahakama ya The Hague kusema kuwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant wanapaswa kukamatwa kwa tuhuma zinazohusiana na vita huko Gaza.

Mwendesha mashtaka pia anatafuta vibalivya kukamatwa kwa viongozi watatu wa Hamas.

Mswada huo uliopendekezwa na Warepublican wanaounga mkono Israel, unalenga maafisa wa ICC waliohusika katika kesi hiyo kwa kuwazuia kuingia Marekani.

Siku ya Jumanne, ilipita kwa wingi wa uungwaji mkono wa Republican kwa kura 247-155. Warepublican wawili walipiga kura ya “waliopo” na Wanademokrasia 42 wanaounga mkono Israel waliungamkono sheria hiyo.

Ingawa mswada huo ulipitishwa katika Bunge, hautarajiwi kuwa sheria.

Sheria hiyo huenda ikapuuzwa na Wanademokrasia wanaodhibiti Seneti ya Marekani, ambapo itabidi ipitishwe kabla ya kutiwa saini na rais kuwa sheria.

Lakini Rais Joe Biden pia amedokeza kuwa “anapinga vikali” mswada huo na utawala umesema hauungi mkono vikwazo hivyo.