Bunge la Japani limemwidhinisha Shigeru Ishiba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Japani kumrithi Fumio Kishida.
Ishiba aliye na umri wa miaka 67 alipata ushindi wa kiti hicho baada ya kuzoa kura 215 kwa tiketi ya chama tawala cha Liberal Democratic (LDP), dhidi ya kura 194 za Sanae Takaichi wa chama cha Consecutive.
Tayari ,Waziri Mkuu huyo amebuni Baraza la Mawaziri 19 huku akikabiliwa na mtihani wa kubuni serikali mpya na kupanga uchaguzi mpya wa ghafla Oktoba 27.
Mabalozi wapya walioteuliwa wanajumuisha wanawake wawili kutoka kwa watano waliokuwa kwenye serikali inayoondoka.
Miongoni mwa mawaziri walioteuliwa ni pamoja na Waziri mwenye mamlaka katika serikali ya zamani Katsunobu Kato ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.